Friday, March 30, 2018

ATUPWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 9

  mtilah       Friday, March 30, 2018

Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Shadrack Majimbo mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa Nakuru nchini Kenya, amehukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 9 na kumuambukiza magonjwa ya zinaa.

Hakimu Judicaster Nthuku amesema kuwa ushahidi unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyo alifanya vitendo hivyo vya ubakaji, na ripoti ya daktari kuthibitisha hilo huku akimuambukiza ugonjwa wa zinaa aina ya ngono.

Mahakama imeelezea kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya binti huyo, ambapo siku ya tukio alimuita na kumtaka kumsaidia kazi za nyumbani, na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili na udhalilishaji.

Sambamba na hilo mwanaume mwengine mwenye umri wa miaka 74 aliyetambulika kwa jina la Kipngeno arap Bor katika eneo la Subukia nchini Kenya huko huko Nakuru, amehukumiwa miaka 10 jela kwa kosa la kumbaka mjukuu wake, ambaye mashahidi walimkuta akifanya tendo hilo baada ya kusikia kelele za binti huyo akilia na kuomba msaada.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post