ZARI ATANGAZA RASMI KUACHANA NA DIAMOND PLATNUMZ...KISA MICHEPUKO MINGI

Zarinah Hassan maarufu kama Zari ama Zari The Boss Lady ametangaza kuachana na mzazi mwenzake, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz kufuatia kuwapo kwa tuhuma nyingi kuhusu mwanamuziki huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana wengine.


Zari ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema kuwa kumekuwapo na tuhuma na wakati mwingine kuna uthibitisho katika mitandao kuhusu tabia ya mara kwa mara ya Diamond kuchepuka, na hivyo ameamua kuachana na kwa sababu heshima yake, utu wake haviwezi kuharibiwa.

Zairi amesema kwamba anaachana na Diamond kama mpenzi wake lakini wataendeleaa kuwa wazazi wenza.

Aidha, katika waraka wake, Boss Lady amesema kuwa, tukio hilo halitapunguza namna anavyowajali wanae, na Zari ambaye amekuwa akifahamika kwa kujituma siku zote.

“Elewa kuwa hiki ni kitu kigumu sana kwangu kukifanya, kumekuwa na tetesi mbalimbali baadhi kati ya hizo zimekuwa na ushaidi ambao umekuwa ukisambaa katika vyombo vya habari kuhusiana na usaliti wa kimapenzi unaofanywa na Diamond, kwa huzuni nimeamua kuvunja uhusiano wangu wa kimapenzi na Diamond kwa heshima yangu”
“Tunaachana kama wapenzi lakini sio kama wazazi hii hainipunguzii mimi kuwa mtu wa kujitegemea, mama mwenye kujali na Boss Lady, wote mnatakiwa kufahamu hilo nitaendelea kujijenga kama mwanamke mwenye ushawishi, nitawaamasisha wanawake wote kuwa maboss Ladies”
“Nitawafundisha watoto wangu wanne wa kiume kuwaheshimu wanawake na nitamfundisha binti yangu ni nini maana ya heshima, nimekuwa katika kiwanda cha burudani kwa miaka 12 sasa pamoja na changamoto zote hizo lakini nimefanikiwa kuwa mshindi kwa sababu mimi ni mshindi nawatakiwa wote siku njema ya wapendanao”

Zari ameandika;

Understand that this is very difficult for me to do. There have been multiple rumors some with evidence floating around in ALL SORTS of media in regards to Diamond’s constant cheating and sadly I have decided to end my relationship with Diamond, as my RESPECT, INTEGRITY, DIGNITY & WELL BEING cannot be compromised.

We are separating as partners but not as parents. This doesn’t reduce me as a self-made individual, and as a caring mother, and the boss lady you have all come to know.

I will continue to build as a mogul, i will inspire the world of women to become boss ladies too. I will teach my four sons to always respect women, and teach my daughter what self-respect means. Unlike many, I’ve been in the entertainment industry for 12 years, and through all my challenges I came out a victor because I am a winner, and so are all of you Zari supporters.


HAPPY VALENTINE’S.
Zari ametangaza uamuzi wa kuachana na Diamond Februari 14,2018 wakati watu wakisherehea siku ya wapendanao, ambapo wengi wameigeuza na kuwa siku ya wapenzi ambapo kila mmoja anajaribu kumuonyesha mwenzake namna anavyompenda kwa kufanya mambo mbalimbali.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Zari na Diamond walianza kudaiwa kuwa hawapo pouwa katika mahusiano yao toka kuvuja kwa  clip video iliyokuwa inadaiwa kuwa Diamond alimpeleka msichana mwingine kulala nae Madale lakini tukio la Diamond kunaswa na camera za mapaparazi akikumbatina na mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu wakati wa utambulisho wa  Mbosso kama msanii mpya wa WCB, kitendo kile kilidaiwa kuwa hakikumpendeza Zari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527