WATU WAWILI WATIWA MBARONI KWA KUHUSIKA NA MAUAJI YA KIONGOZI WA CHADEMA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Slaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya aliyekuwa Kiongozi wa chama cha Chadema Kata ya Hananasifu, Marehemu Daniel John.

Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa alisema watu hao walikamatwa majira ya saa nne usiku, Februari 23 mwaka huu maeneo ya Hananasifu Kinondoni.

“Kufuatia uchunguzi unaoendelea juu ya mauaji hayo, walikamatwa watu wawili mmoja jinsia ya kike na mwingine wa kiume,” alisema.

Mwili wa marehemu Daniel John uliokotwa maeneo ya Coco Beach jijini Dar es Salaam, ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni, ilisema mwili wa John ulikutwa na majeraha sehemu za mikono, miguu na kichwani yanayoashiria kwamba alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post