RAIS MAGUFULI AMWAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI NA NAIBU WAKE,MAJAJI WAWILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaapisha Majaji 2, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliowateua tarehe 01 Februari, 2018.

Walioapishwa kuwa Majaji ni Mhe. George Mcheche Masaju na Mhe. Gerson John Mdemu.

Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Dkt. Adelardus Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mhe. Paul Joel Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Matukio yote mawili yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.