MKE AFARIKI KWA KUGONGWA NA TRENI AKIPIGA 'SELFIE' NA MUMEWE KWENYE RELI

Leo Februari 9, 2018 kuna hii ya kuifahamu kuhusu Mwanamke mmoja baada ya kunywa pombe na kulewa huku wakifurahia wakati waliokuwa nao, kwenye Mji wa Bangkon nchini Thailand akiwa na rafiki yake amegongwa na kupoteza maisha huku mwenzie akijeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na treni walipokuwa wanapiga ‘selfie’.

Rafiki huyo ambaye amejeruhiwa ameelezea mkasa huo na kusema walikuwa wamekunywa pombe na kulewa na ndiyo Marehemu akamwambia wakapige picha kwenye reli lakini hawakuwa wameona treni inayokuja upande mwingine.

Tukio hilo lilitokea katika kituo cha treni cha Samsen February 8, 2018 na inaelezwa kuwa binti huyo aliyefariki alikuwa ana miaka 24 na aliumia vibaya mguu na alipoteza maisha akiwa anapatiwa matibabu hospitali.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.