Tanzia : MWENYEKITI WA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MTWARA HASSAN SIMBA AFARIKI DUNIA


Hassan Simba enzi za uhai wake
Habari zilizotufikia hivi punde zinaarifu kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (Mtwara Press Club) Hassan Simba amefariki dunia katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam leo mchana Jumamosi Februari 24,2018.

Hassan Simba ambaye alikuwa anaandikia gazeti la Habarileo amefariki alipokuwa anapata matibabu baada ya kuugua muda mrefu.

Mungu ailaze Mahali Pema Peponi roho ya Marehemu Hassan Simba. Amina! 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527