BABU WA MIAKA 75 AUAWA NA KUCHUNWA NGOZI SONGWE


Mzee mmoja aliyetambulia kwa majina ya Tuntinala Kunyepa (75) mkazi wa Kijiji cha Ihanda Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, amekutwa akiwa ameuawa na kuchunwa ngozi na kisha kutolewa baadhi ya viungo vya mwili wake na watu wasiojulikana .

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, Yusuph Sarungi, amesema, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Januari 31,2018 na kwamba, hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hiilo huku mauaji hayo yakihusishwa na imani za kishirikina ambapo uchunguzi na msako mkali unaendelea kuwabaini waliohusika.
Chanzo - EATV
Theme images by rion819. Powered by Blogger.