Maajabu haya!! MWANAMKE AJIFUNGUA KOPO BADALA YA MTOTO MWANZA






Na Jesse Mikofu, Mwananchi 

Veronica Paschal (29) mkazi wa Kishili jijini Mwanza ametolewa kopo la mafuta ya kujipaka mwilini katika sehemu za siri, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuwaeleza ndugu zake kuwa anataka kujifungua kopo.


Licha ya kutolewa kopo hilo, daktari aliyekuwa zamu katika kituo cha afya Igoma jijini hapa, Zaitun Lionge ameeleza kuwa mimba ya miezi sita ya mwanamke huyo ipo salama.


Tukio hilo la aina yake limetokea Januari 17, 2018 baada ya Veronica kufikishwa katika kituo hicho cha afya na ndugu zake waliomtoa kwenye zahanati binafsi.


“Mwanzoni hawakuonyesha ushirikiano ndio tukawambia tutafanyaje. Wakasema kuna kopo kwamba ndugu yao anataka kujifungua kopo, tukauliza kopo linazaliwaje? Amehoji na kuongeza,


“Tukawambia hilo kopo halijaingia lenyewe mtakuwa mmeliweka wenyewe. Kopo lilikuwa halionekani lakini anavyojaribu kusukuma likatokezea.”


Amesema walipomchunguza kwenye vipimo ndipo walipolibaini kopo hilo la mafuta ya kujipaka mwilini, kwamba baada ya kulitoa waliita Polisi kuchukua maelezo ya mhusika na ndugu zake.


Amesema ujauzito wa mwanamke huyo uko salama kutokana na njia kutofunguka baada ya kuondolewa kopo hilo.


Mwananchi linaendelea kumtafuta mwanamke huyo wa taarifa zaidi.

Chanzo- Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527