PATRICK SOSOPI NDIYO MRITHI WA KATAMBI ALIYETIMKIA CCM


Kamati ya Utendaji ya Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) limemchagua Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo kuchukua nafasi ya Patrobasi Katambi aliyehamia Chama cha Mapinduzi.


Kamati hiyo pia leo Desemba 2 imetangaza kuziba nafasi ya nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kumteua John Pambalu, nafasi iliyoachwa wazi na Sosopi. Viongozi hao wameteuliwa kuongoza baraza hilo kwa muda wa mwaka mmoja.


Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita amesema uamuzi huo ulifanyika jana kufuatia kikao cha dharura cha kamati hiyo ya utendaji.


Amesema baraza hilo ni mojawapo ya taasisi imara na itaendeleza mapambano."Tunawahimiza vijana wa Chadema na vijana wote wa Tanzania wasimame kidete kwenye kazi ya kuijengea na kuipigania demokrasia ya nchi yetu katika misingi ya utawala bora na haki za binadamu,"


Kwa upande wake Ole Sosopi amesema katika uongozi wake atahakikisha baraza hilo linarudi kwenye misingi imara na kuongoza mapambano ya kudai demokrasia.


Amesema akiwa mwenyekiti hatavumilia kuendelea kuona uonevu wanaofanyiwa wanachama wa Chadema.


"Bavicha inaenda kuwa taasisi bora na imara zaidi baada ya kuondoka Katambi. Tunakwenda kupambania Demokrasia a, tutawashawishi vijana kuwa wamoja kulitetea taifa bila kujali maslahi ya vyama," amesema Ole Sosopi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post