SIMBA YAWEKA KAMBI SUMBAWANGA


Kikosi cha Simba kimeamua kuhamishia kambi yake mjini Sumbawanga mkoani Tanga.

Simba ambayo ilikuwa Katavi ambako ilicheza mechi ya kirafiki na kutoka sare ya 0-0, sasa imehamia mjini Sumbawanga na kuanzisha kambi.

Kambi ya Simba mjini Sumbawanga itaendelea hadi Jumamosi itakapocheza na Rukwa FC ikiwa ni mechi nyingine ya kirafiki.

Baada ya mechi hiyo, Simba itafunga safari kurejea Mbeya kufanya maandalizi yake ya mwisho dhidi ya Prisons ya Mbeya.

Simba itaanza kujifua leo alasiri kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, uwanja ambao utatumika katika mechi yao dhidi ya Rukwa FC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527