MBUNGE GODBLESS ATAKA WABUNGE WA CUF YA LIPUMBA WAONDOLEWE BUNGENI

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemshauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kutumia busara kuwaondoa bungeni wabunge nane walioingia bungeni kuziba nafasi za wabunge nane waliokuwa wamevuliwa uanachama wa chama cha CUF Julai 24.



Lema ametumia mtandao wake wa kijamii kuandika ujumbe huo ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama Kuu kutengua uamuzi wa kufukuzwa kwa Wabunge 8 na Madiwani 2 wa Chama cha Wananch CUF mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa.


“Mh Spika anapaswa, kuzingatia kwa busara uamuzi uliotolewa na mahakama kwa kuwaondoa wale Wabunge wa Lipumba ndani ya Bunge na kuwarejesha Wabunge halali sasa, Mpaka hapo haki itakaposhinda zaidi,”ameandika Lema



Wabunge hao nane walivuliwa uanachama Julai 24 na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi, CUF linaloongozwa na Prof. Lipumba kwa madai ya utovu wa nidhamu yakiwemo kukisaliti chama hicho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527