Angalia picha : MAHAFALI YA TISA YA KIDATO CHA NNE KOM SEKONDARI MWAKA 2017 SHINYANGA

Shule ya Sekondari Kom iliyopo mjini Shinyanga leo Jumamosi Novemba 11,2017 imefanya mahafali ya tisa ya wahitimu wa elimu ya kidato cha nne mwaka huu 2017 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2006.

Mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya kidato cha nne mwaka 2017 yaliyohudhuriwa na wazazi na wageni mbalimbali alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.


Akizungumza katika mahafali hayo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema mabadiliko yoyote yanaletwa na ushirikiano hivyo kupitia ushirikiano

Alisema shule hiyo imekuwa maarufu nchini kutokana na elimu bora inayotoa na kutokana na hali  hiyo imeupatia sifa mkoa wa Shinyanga.

“Sisi kama serikali tunajivunia uwepo wa shule hii katika mazingira yetu kwani inatutangaza, tupo tayari kushirikiana nanyi katika kutatua changamoto zinazojitokeza ili kusukuma gurudumu la maendeleo”,alieleza Matiro.

“Tupo tayari kuhakikisha kuwa tunashirikiana na sekta binafsi na milango yetu ipo wazi na panapotokea changamoto msisite kutufikia”,alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wazazi kuwekeza kwenye elimu kwa watoto kwani huo ndiyo urithi wenye thamani katika maisha yao.

Katika hatua nyingine aliipongeza shule hiyo kuajiri watu 63 katika shule kwani wanaunga mkono lengo la serikali la kuzalisha ajira kwa wananchi.


Aidha aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuanzisha shule ya awali na msingi kitendo ambacho kinatokana na ushirikiano uliopo kati ya shule na wazazi ambao wamekuwa mstari wa mbele kusukuma maendeleo ya shule.

Matiro aliwataka wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kuwa mfano katika maeneo wanakokwenda na kuhakikisha matendo yao yanaendana na mambo waliyofundishwa shuleni.

Naye Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari Jackton Koyi aliishukuru serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiwapa katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inafikia malengo yake.

Alisema Kom sekondari shule hiyo imetimiza miaka 12 tangu kuanzishwa kwake na imekuwa daraja la elimu kwa wanafunzi ambao wengi wamekuwa wakiingia kidato cha tano na kujiunga katika vyuo mbalimbali.

“Shule yetu imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani,mfano kati ya wanafunzi 160 waliomaliza kidato cha nne mwaka 2015,145 walijiunga na masomo ya kidato cha tano,na mwaka 2016 kati ya wanafunzi 144 waliofanya mtihani wa kidato cha nne,133 walijiunga kidato cha tano”,aliongeza Koyi.

“Naomba wazazi muendelee kutuamini na kuleta wanafunzi katika shule hii ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani mbalimbali”,alieleza Koyi.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo,Mwita Warioba alisema shule hiyo hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 542,walimu 32 huku akisisitiza kuwa lengo la shule hiyo ni kutoa elimu bora na tayari shule hiyo pia imeanzisha shule ya awali na msingi.

“Shule yetu ina miundo mbinu ya kutosha,madarasa yapo ya kutosha,tuna umeme wa Tanesco,maji kutoka ziwa Victoria,mabweni 8,viwanja vya michezo,maktaba moja,maabara mbili ikiwemo ya Computer”,aliongeza Waryoba.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne,Jackline Benson alisema walianza kidato cha kwanza wakiwa 104,ambapo wavulana walikuwa 52 na wasichana 52 lakini idadi iliongezeka na hivyo idadi ya waliohitimu kidato cha nne mwaka huu ni 154,kati yao wasichana ni 73 na wavulana 81.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha za matukio yaliyojiri wakati wa mahafali hayo angalia hapa chini 
Wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2017 katika shule ya sekondari Kom wakimpokea mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya shule hiyo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 
Mkurugenzi wa shule ya sekondari Kom,Jackton Koyi akimpokea mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa ajili ya kushiriki mahafali ya kidato cha nne katika shule hiyo 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwapungia mkono wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kom 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya mkurugenzi wa shule ya sekondari Kom 
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Zena Ali akimweleza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro historia ya shule ya sekondari Kom wakati wa maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika shule hiyo 
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kom wakionesha ramani ya dunia kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati wa maonesho ya taaluma wakati wa mahafali hayo 
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Rajuu Masudi ambaye ni mtaalamu wa kuchora akieleza kuhusu sanaa ya uchoraji inayofanywa na wanafunzi wa shule ya sekondari Kom 
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kom,Safia Ali akitoa maelezo kuhusu maonesho ya sayansi kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro 
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikata utepe wakati wa mahafali ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kom.Kulia ni mwenyekiti wa bodi ya shule Peter Kugulu,kushoto ni mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi 
Kijana wa skauti akimvalisha skafu mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati wanafunzi waliohitimu kidato cha nne wakiandamana kuelekea kwenye ukumbi wa sherehe ya mahafali hayo 
Wahitimu wa kidato cha nne 2017 katika shule ya sekondari Kom wakiandamana 
Wahitimu wakiandamana kuelekea ukumbini
Wahitimu wakiingia ukumbini 
Meza kuu wakipokea maandamano ya wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kom 
Mkuu wa shule ya sekondari Kom,Mwita Waryoba akielezea historia ya shule hiyo
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi akizungumza wakati wa mahafali ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kom 
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi akizungumza 
Wahitimu wa kidato cha nne wakiwa ukumbini 
Wahitimu wa kidato cha nne wakipunga mkono 
Wahitimu wakiwa ukumbini 
Wahitimu wakiwa ukumbini 
Walimu wa shule ya sekondari Kom wakiwa kwenye mahafali 
Wahitimu wa kidato cha nne,Scholastica Simon na Dickson Nyansika wakikata keki wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwaka 2017 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimlisha keki mhitimu wa kidato cha nne Dickson Nyansika 
Scholastica Simon na Dickson Nyansika wakimlisha keki mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro 
Dickson Nyansika akimlisha keki Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi 
Wazazi wakiwa katika mahafali hayo 
Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea 
Wazazi wakiwa eneo la tukio 
Mzazi akifurahia jambo 
Mahafali yanaendelea 
Mahafali yanaendelea 
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom (kushoto) ,Jackton Koyi na mke wake Magreth Jackton Koyi (kulia),wakipokea zawadi ya keki iliyoandaliwa na wazazi ,Ibrahim Okero na Lucia Ibrahim Okero (katikati) kwa ajili ya viongozi wa shule ya sekondari Kom kutokana na mchango wanaotoa katika sekta ya elimu

Mahafali yanaendelea
Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea 
Baadhi ya wanafunzi wanaobaki katika shule hiyo wakiwa kwenye mahafali hayo 
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kom wakiimba wimbo 
Wahitimu wa kidato cha nne, Jackline Benson na Kelvin wakisoma risala 
Vijana wa skauti wakitoa burudani 
Mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Samwel akitoa burudani ya wimbo 
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Kom Peter Kuguru akizungumza katika mahafali hayo 
Wanafunzi wakionesha ubunifu wa mavazi 
Wanafunzi wakiwa wamevaa mavazi mbalimbali ya ubunifu 
Wanafunzi wakiimba shairi 
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa mahafali ya 9 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kom 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa mahafali hayo 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza 
Wageni waalikwa wakiwa katika mahafali hayo 
Ma Dj wakiwa eneo la tukio
Mgeni rasmi Josephine Matiro akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia kupatikana kwa samani katika bweni la wasichana katika shule ya sekondari Kom ambapo shilingi milioni 9 zinahitajika 
Akina mama wakiwa katika foleni kwenda kuchangia fedha kwa ajili ya samani za ndani katika bweni la wanafunzi
Harambee inaendelea
Akina baba wakiwa katika foleni kuchangia fedha kwa ajili ya samani katika bweni la wanafunzi
Harambee inaendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akishikana mkono na wageni waalikwa wakati wa harambee hiyo

Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA),Nsianeli Gelard akizungumza wakati akitoa mchango uliotolewa na SHUWASA kwa ajili ya kununua samani katika bweni la wasichana katika shule ya sekondari Kom

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga,Said Pamui akizungumza wakati akitoa mchango uliotolewa na SHUWASA kwa ajili ya kununua samani katika bweni la wasichana katika shule ya sekondari Kom

Walimu wa shule ya sekondari Kom wakicheza wakati wa mahafali hayo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa zawadi ya fedha kwa mmoja wa walimu katika shule ya sekondari Kom
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa vyeti kwa wahitimu
Zoezi la kugawa vyeti likiendelea
Wahitimu wakiwa katika foleni kupokea vyeti
Wahitimu wakijiandaa kupokea vyeti ya kuhitimu kidato cha nne.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527