WAZIRI UMMY AIBEBA AFRICAN SPORTS YA JIJINI TANGA


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na wachezaji wa timu ya African Sports kabla ya kuwakabidhi hundi milioni 2.1 leo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi nahodha wa timu ya African Sports hundi ya milioni 2.1 leo wanaoshuhudia ni viongozi na wachezaji wa timu hiyo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya African Sports leo mara baada ya makabidhiano hayo.
Mmoja kati ya viongozi wa timu ya African Sports akimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo
Waziri  wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo
***
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewakabidhi timu ya African Sports “Wana kimanu manu” shilingi
milioni 2.1 kwa ajili ya posho za wachezaji wa timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la pili Tanzania.


Licha ya kukabidhi fedha hizo,pia amewalipia kwenye shirikisho la soka Tanzania (TFF)Laki tano (500,000) kwa ajili ya leseni za wachezaji na ada ya ushiriki wa timu hizo.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada
huo,Waziri Ummy alisema ameamua kutoa msaada huo ili kuiwezesha tmu hiyo kuweza kutimiza malengo yake ikiwemo kupanda daraja na kufikia hatua ya kucheza Ligi kuu soka
Tanzania Bara.

“Kwani iwapo timu hiyo itarejea Ligi kuu
soka Tanzania Bara itasaidia kukua kwa fursa mbalimbali za kiuchumi katika Jiji la Tanga.

"Sambamba na hilo lakini pia tumepokea
mchango wa milioni 3 kutoka Kampuni ya GBP Oil ya Tanga ambao umeweza kuipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano wanayowakabili",alisema.


Aidha aliitaka timu hiyo
wahakikishe wanafanya vizuri katika michuano hiyo ili kuweza kurejesha hadhi yake ya miaka ya nyuma ilipoweza kuwika katika medani ya soka hapa
nchini.

“Ndugu zangu wana African Sports
msituangushe hakikisheni mnatumia misaada hii mnayoipata iweza kuwa chachu ya kufikia malengo yenu ya
kufanya vizuri “,alisema.

Hata hivyo pia Waziri Ummy aliwafungulia
akaunti ya fedha wachezaji wote wa timu hiyo katika benki ya NMB ili iwe rahisi posho zao kulipwa moja kwa moja kupitia benki ili kuepusha migogoro inayoweza
kujitokeza.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post