WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KARIAKOO WAPEWA ZAWADI NA BENKI YA NIC KUFURAHIA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA


Meneja wa idara ya Wateja wadogo na taasisi wa benki ya NIC, Natasha Cathles akiwashukuru wanawake wajasiriamali pamoja na wateja wengine kwa kuwa wateja wao na hatimaye kutoa zawadi kwa Wanawake wajasiriamali hao ikiwa ni ishara ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
Mkuu wa tawi la benki ya NIC lililopo Kariakoo, Majid Mohamed akiongea na wanawake wajasiriamali (hawapo pichani) waliofika katika tawi hilo kwa ajili ya kukabidhiwa zawadi ikiwa ni ishara ya benki hio kutoa shukrani kwa wateja wake huku ikiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mmoja wa wateja na mwanamke mjasiriamali wa Kariakoo, Bi Lucia Mlimi akiwashukuru wafanyakazi wa benki ya NIC tawi la Kariakoo na uongozi kwa ujumla kwa kuona mchango wao na kuamua kuwatunuku zawadi mapema leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
Wanawake wajasiriamali wakipokea zawadi zao leo
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa wanawake wajasiriamali hao


Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NIC wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali wa Kariakoo ambao wamepewa zawadi na benki hio ikiwa ni ishara ya kutoa shukrani kwa wateja wao na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
Wanawake wajasiriamali wa Kariakoo pamoja na mfanyakazi wa benki ya NIC wakikata keki kuashiria maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja na kufurahi pamoja na wanawake hao kwa kuwapa zawadi
Baadhi ya wanawake wajasiriamali waliopokea zawadi kutoka Benki ya Nic mapema leo.

Picha Zote na Josephat Lukaza | Lukaza Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post