WANAFUNZI 385,938 KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KUANZIA KESHO OKTOBA 30

Watahiniwa 385,938 wanatarajiwa kutafanya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne nchini.


Akizungumza leo Jumapili, Oktoba 29,2017 Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa hao, 323,513 ni wa shule na 62,425 ni wa kujitegemea.


Dk Msonde amesema mtihani huo utaanza kesho Oktoba 30,2017 hadi Novemba 17,2017.


Dk Msonde amesema maandalizi ya mitihani yameshakamilika."Hivi ninavyozungumza mitihani imeshafika kwenye vituo.”


Amezitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unafuatwa.


Katibu mtendaji huyo amewataka wanafunzi kuacha vitendo vya udanganyifu wakati wa kufanya mitihani kwa kuwa wanaweza kufaulu bila kufanya hivyo.


"Mliyojifunza yanatosha fanyeni mitihani kwa kufuata utaratibu uliowekwa," amesema.


Dk Msonde amesema baraza hilo halitasita kuwafutia mitihani wote watakaojihusisha na udanganyifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527