Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu amefanywa upasuaji mara 14 na ataendelea kufanyiwa upasuaji
mwingine wa 15 ndani ya wiki mbili zijazo.
Mbowe
amesema hayo jana kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi
wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.
Alisema
hali ya Lissu inaendelea kuimarika lakini aliumizwa sana kama
walivyokuwa wanaeleza mara zote lakini na jambo la kumshukuru Mungu
kwamba ameendelea kuimarika.
"Ameendelea
kupata afya, akili zake ni timamu, madaktari kule wanafanya kazi kubwa
kwelikweli kuendelea kumuudumia na ni matumaini yetu kuwa baada ya muda
Mungu atamrejesha katika wajibu wake wa kulitumikia Taifa,"
Mbowe
alizungumza hayo baada ya kueleza kuwa alitokea Nairobi kuangalia afya
ya mbunge huyo ambaye alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu akiwa
nyumbani kwake mjini Dodoma.