Tanzia : MWANDISHI WA HABARI ANCETH NYAHORE AFARIKI DUNIA


Mwandishi wa habari Mwandamizi nchini Tanzania Anceth Andrew Nyahore amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Sekouture jijini Mwanza.

Nyahore amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Oktoba 22,2017.

Nyahore alikuwa akiandikia  gazeti ya Nipashe,The Guardian na Zanzibarleo.

Nyahore pia aliwahi kufanya kazi na ITV na Radio One.

Taarifa za kifo cha Nyahore zimethibitishwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Simiyu Frank Kasamwa na kwamba taarifa zaidi kuhusu msiba zitatolewa.

Kabla ya kuhamia mkoani Simiyu,Nyahore alikuwa anafanya shughuli za uandishi wa habari mkoani Shinyanga.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Anceth Nyahore.Amina. 

Nyahore enzi za uhai wake akitekeleza majukumu yake


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post