TGNP MTANDAO KUFANYA TAMASHA KUBWA LA JINSIA KUANZIA SEPTEMBA 5-8,2017 JIJINI DAR ES SALAAM


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP, Vicensia Shule (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana kuzungumzia Tamasha la Jinsia la mwaka 2017 linalotarajia kuanza rasmi Septemba 5 hadi 8 ya mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa FemAct, Abdulla Othman.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP, Vicensia Shule (katikati) akijibu maswali anuai ya waandishi wa habari kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi na Mwenyekiti wa FemAct, Abdulla Othman.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (katikati) akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano na vyombo vya habari kuzungumzia Tamasha la Jinsia la mwaka 2017 linalotarajia kuanza rasmi Septemba 5 hadi 8 ya mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP, Vicensia Shule pamoja na wanaharakati wengine.
****
MTANDAO ya Jinsia Tanzania (TGNP) umeweka hadharani malengo makuu ya Tamasha la Jinsia la mwaka 2017 linalotarajia kuanza rasmi kesho Septemba 5 hadi 8 mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP, Vicensia Shule alisema tamasha la mwaka huu litakuwa na malengo manne ambapo lengo la kwanza ni kutafakari na kusherehekea mafanikio, changamoto zilizopo katika kuendeleza usawa wa kijinsia. 

Alisema lengo hilo ni katika akuzingatia utekelezaji wa mikataba, maazimio, sera na mikakati mbalimbali ya kimataifa.

Alilitaja  lengo la pili kuwa ni kutathmini ushiriki wa wanawake katika michakato ya kufanya maamuzi katika uongozi, hususan uongozi wa kisiasa kwenye Serikali za mitaa.

 Lengo la tatu ni pamoja na kufuatilia kuhifadhi, kutambua na kusherehekea viongozi wanawake wenye michango ya kuigwa juu ya usawa wa kijinsia na uwezo wa wanawake, hususan mapambano dhidi ya mfumo dume na uliberali mamboleo.

Akifafanua kuhusiana na lengo la tatu, Shule alisema katika lengo hilo TGNP itawatambua na kuwapongeza wanawake waliofanya vizuri maeneo mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu, Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anna Makinda, Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, Mama Getrude Mongela, Dk. Ester Mwaikambo na Msanii Fatma Baraka (Bi. Kidude) kwa jitihada walizozionesha katika uongozi.

Aidha alisema lengo la nne itakuwa kuhimarisha harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi kupitia ujenzi wa nguvu za pamoja. “…Tamasha la Jinsia la mwaka huu litaongozwa na mada kuu isemayo ‘Mageuzi ya mifumo kandamizi kwa usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu” alisema Shule.
Mwenyekiti wa asasi ya WAJIKI, Janeth Mawinza (katikati) pamoja na wanaharakati wengine akifafanua jambo kwa wanahabari katika mkutano huo.
Mwanaharakati, Seleman Bishagazi (katikati) pamoja na wanaharakati wengine akifafanua jambo kwa wanahabari katika mkutano huo.
Sehemu ya wanahabari wakifuatilia mazungumzo hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post