MSICHANA AJIUA BAADA YA KUTOLEWA NJE YA DARASA NA MWALIMU KISA DAMU YA 'HEDHI'


Msichana wa umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi kusini mwa India amejiua baada ya mwalimu wake kumuaibisha kwa sababu ya hedhi.

Katika ujumbe alioacha wakati wa kujiua, alidai mwalimu wake "alimtesa".

Ingawa msichana huyo hakutaja kisa hicho cha kuaibishwa kwa sababu ya hedhi, mamake msichana huyo anasema aliagizwa na mwalimu wake kutoka nje ya darasa baada kwa sababu ya doa la damu ya hedhi lililokuwa kwenye nguo zake.

Hedhi ni mwiko kuzungumziwa hadharani India.

Wanawake kitamaduni huaminika kuwa wachafu au hata waliolaaniwa wakati wanapopata hedhi.

Polisi wanasema wamepata ripoti za kisa hicho cha kujiua na wanafanya uchunguzi.

Kisa hicho kilitokea Jumapili katika wilaya ya Tirunelveli siku ya Jumapili katika jimbo la Tamil Nadu.

"Sijui ni kwa nini mwalimu wangu analalamika kunihusu. Bado sielewi ni kwa nini ananihangaisha na kunitesa hivi," mwanafunzi huo aliandika kwenye barua yake.

Alianza barua hiyo: "Amma (mama), tafadhali nisamehe."

Mamake mwanafunzi huyo anadai mwalimu huyo alimchapa binti yake siku za awali kwa kutofanya kazi yake ya ziada.

"Binti yangu alipata hedhi akiwa shuleni Jumamosi iliyopita," mamake ameambia BBC Tamil.

"Alipomjulisha mwalimu wake, alipewa kitambaa cha kupangusa ubao atumie kama sodo.

"Mwalimu alimfanya binti yangu kusimama nje ya darasa. Msichana wa miaka 12 atavumiliaje aibu ya aina hiyo?" alishangaa.

Msichana huyo alijiua siku moja baadaye.

Shule hiyo imeambia BBC kwamba inashirikiana na polisi katika uchunguzi.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post