![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvaMUBpaHbcPvAYj6tFPsB9JoyJyI4azI5-O_As7OV-XK4QA2HIEa82atKZTu3FJOMP3MtCXuyqGFYSrzNhTouCPPogl0ihZ7Xh53VNayrhi7YHyDx0JMx8BWkfk0Kx2zWjnVtOJlTLXrH/s640/tmp_12101-1-2-2081881050.jpg)
Katika akaunti yake ya Twitter, Rais Magufuli amesema anamuombea Lissu kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka.
“Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria,” amesema.
Lissu amejeruhiwa leo Alhamis akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D na sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.