JWTZ YATOA TAARIFA KUHUSU MWANAJESHI ALIYEUAWA CONGO


Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa mwili wa marehemu Praiveti Mussa Jumanne Muryery ambaye ameuawa nchini DRC akiwa katika jukumu la Ulinzi wa Amani, utaagwa kwa heshima tarehe 25 Septemba 2017 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kuanzia saa 2:00 asubuhi.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Florens M. Turuka ataongoza katika kuuaga mwili wa Marehemu.


Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi Amin.


Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
22 Septemba, 2017.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527