BINTI ABAKWA HADI KUFA KINONDONI DAR ES SALAAM

Kundi la vijana wasiofahamika wamembaka msichana wa miaka 20 hadi kufa na kisha kumtupa jalalani maeneo ya jirani na nyumbani kwao Madale Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 

Wakisimulia tukuio wazazi wa binti huyo, wamesema kuwa mpaka majira ya saa nne usiku kuamkia Jana Septemba 7 alikuwa nyumbani kabla ya kuwasili kwa vijana watatu waliokuja na pikipiki (bodaboda) na kuanza kuzungumza naye kama marafiki kwa takribani saa nzima na baadae binti yake kuaga akitaka kuwasindikiza na hakurudi tena hadi alipopewa taarifa za kifo hicho. 

Aidha Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Madale, Gration Mbelwa ameliomba Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kuwaomba wanafamilia pamoja na rafiki za binti huyo kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwakamata watuhumiwa hao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post