BENKI YA CRDB YATOA ELIMU YA FEDHA NA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI TINDE - SHINYANGA


Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akizungumza wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.
***

Benki ya CRDB leo Jumatano Septemba 20,2017 imeendesha mafunzo ya ujasiriamali,elimu ya fedha na mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali waliopo katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.

Mafunzo hayo yaliyokutanisha pamoja wajasiriamali zaidi ya 500 yamefanyika katika ukumbi wa Mountain View Hotel iliyopo Tinde ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM).

Akifungua mafunzo hayo,Mheshimiwa Azza Hilal alisema mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa Tinde kutumia vyema mikopo wanayopata katika taasisi za kifedha hali itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Aidha Mhe. Hilal aliwataka wananchi kuacha tabia ya kukaa na fedha ndani na kukopa pesa kwa watu binafsi kwa riba inakuwa kubwa matokeo yake wanashindwa kuona faida ya biashara wanazofanya.

“Niishukuru benki ya CRDB kwa kuwafikia wananchi wa Tinde,Tinde ni kata inayokua kwa kasi kubwa,naamini wananchi mtatumia fursa ya benki hii kupata huduma za kibenki,naomba Benki ya CRDB iendelee kufungua matawi katika maeneo mengine lakini pia mtoe elimu hii mnayotoa kwa wananchi",alisema mbunge huyo.

Naye Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui alisema mafunzo hayo ni kwa ajili ya vikundi vidogo vya ujasiliamali ambapo benki hiyo inawapa wananchi uelewa wa jinsi ya kujisimamia wenyewe ili kujikwamua kiuchumi.

"Tumekutanisha pamoja wajasiriamali zaidi ya 500,kwa ajili ya kuwapa elimu ya ujasiriamali,elimu ya fedha na elimu bora ya mikopo Kubwa tumewasisitiza namna ya kusimamia biashara zao ili zisimamie,jinsi ya kuzitumia taasisi za fedha ili kupata utaalamu wa kuendesha biashara zao",alieleza Pamui.

“Tumefika hapa kuitikia wito wa wananchi waliokuwa wanahitaji benki ya CRBD ifungue tawi lake Tinde,sisi tupo katika mwendelezo wa kufungua benki katika maeneo ya vijijini na kila tunapofungua matawi, tunatoa elimu kwa wananchi jinsi ya kutumia vizuri taasisi za kifedha”,aliongeza Pamui.

Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa wajasiriamali katika ukumbi wa Mountain View hotel katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.
 Wajasiriamali wakiwa ukumbini
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akiteta jambo na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui
Wajasiriamali wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui akitoa mada ukumbini


Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Tinde Dorcas Ngoye akizungumza ukumbini.





Wajasiriamali wakiwa ukumbini
Picha zote na Said Nassor

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527