MAAFISA WA WIZARA YA USHIRIKIANO WA MAENDELEO YA UJERUMANI WATEMBELEA MAHAKAMA YA AFRIKA


Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR)Sukhdev Chatbar(kulia)akiwaongoza wageni kutoka Wizara  ya ushirikiano wa maendeleo ya Ujerumani kupitia taasisi zake GIZ na AGA waliotembelea mahakama hiyo wamekua ni wadau wakubwa katika kusaidia miradi mbalimbali ya mahakama hiyo. 
Mkutubi wa Maktaba ya mahakama hiyo,Revina Moshi akizungumza na maafisa kutoka
shirika la maendeleo ya kimataifa ya Ujerumani(GIZ),kutoka kushoto ni 
Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa 
Afrika(AU) ofisi ya Addis Ababa,Ethiopia,Barbara Schaefer,Janina Hasse 
kutoka Berlin,Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs 

Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs akiangalia sehemu ya machapisho kwenye maktaba ya AfCHPR. 
Msajili wa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert 
Enno(kulia)akizungumza na ujumbe kutoka taasisi za Wizara ya maendeleo 
ya Ujerumani waliotembelea mahakama hiyo. 
Msajili wa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert Enno akimkabidhi zawadi Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa Afrika(AU) ofisi ya Ethiopia,Barbara Schaefer. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527