JUMBA LA MBUNGE WA CHADEMA, MSANII PROFESA J LAPIGWA X....KUBOMOLEWA MUDA WOWOTE

Msanii wa muziki, ambaye ni Mbunge wa Mikuni kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA, Joseph Haule maarufu kama Professa Jay, yupo matatani kukosa hifadhi ya jumba lake la kifahari alilojenga pembezoni mwa barabara ya Morogoro maeneo ya Mbezi Luis, kwani ni miongoni mwa nyumba ambazo zimewekewa alama ya X kuashiria zipo katika hifadhi ya barabara.Nyumba za kifahari zilizojengwa pembezoni maeneo ya Kimara mpaka Kiluvya jijini Dar es salaam zimekumbwa na bomoabomoa kitu ambacho kimeumiza watu wengi sana, kwani wapo ambao hawana makazi na hawaelewi nyumba zao zikibomolewa wataanzia wapii na wataishi wapi.


Na nyumba ya Mbunge wa Mikumi ni moja ya nyumba ambazo zimewekewa X kuashiria nayo imo miongoni mwa nyumba za kubomolewa.


Hivi karibuni Tanroads imetangaza kuwa muda wowote itaanza utekelezaji wa kubomoa nyumba zilizowekewa alama ya X katika barabara hiyo kupisha ujenzi wa barabara kubwa ya kisasa.


Tayari Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limeshaanza kukata umeme kwenye nyumba nyingi hivyo kuwafanya baadhi ya wenye nyumba kubomoa wenyewe kwa hiari na kufungasha mizigo yao.


Tazama picha ya nyumba ya kifahari ya mbunge wa Chadema Joseph Haule maarufu kama Profesa jay ambaye hivi karibuni alifunga harusi kubwa na kuweka jiko ndani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post