Picha : AJALI YA COASTER KUGONGA TRENI YAUA WATU KADHAA MOROGORO



Watu ambao idadi yake haijaweza kufahamika mara moja, wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya daladala waliyokuwa wakisafiria kugonga treni mkoani Morogoro.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Urich Matei, amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi na imehusisha gari aina ya daladala yenye amba za usajili T 438 ADR iliyokuwa inakwenda Mvumi kwenye njia panda inayoingilia treni ndipo ikagonga treni hiyo, na kuburuzwa takribani mita 200.

Kamanda Matei amesema chanzo cha ajali hiyo ni daladala kuingia kwenye njia ya treni bila kusimama ili kuangalia kama kuna treni inakuja, ndipo treni hiyo ikaburuza gari hiyo kwa umbali mrefu na kusababisha maafa hayo.

Taarifa za awali ni zinasema watu watatu wamefariki dunia na engine kadhaa kujeruhiwa ingawa idadi rasmi ya vifo na majeruhi bado haijafahamika rasmi mpaka sasa na majeruhi wamepelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post