WAZIRI WA USALAMA KENYA AFARIKI DUNIA

Jenerali Joseph Ole Nkaissery

Waziri wa usalama wa Kenya Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery amefariki dunia.

Waziri huyo amefariki dunia saa chache baada yake kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Bw Joseph Kinyua mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.

"Ni kwa huzuni kubwa na mshangao kwamba tunatangaza kifo cha ghafla cha Waziri wa Usalama wa Ndani Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery," taarifa ya Bw Kinyua imesema.

"Taifa litaendelea kupashwa habari zaidi punde maelezo yatakapopatikana."

Jenerali Nkaissery amefariki siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe G.G Gitahi aliyekuwa seneta wa jimbo la Laikipia kufariki dunia.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post