RAIS WA TFF JAMAL MALINZI NA KATIBU WAKE WANYIMWA DHAMANA,WARUDISHWA RUMANDE


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamenyimwa dhamana kwa kesi inayowakabili, wamerudishwa rumande mpaka Julai 17 mwaka huu shtaka lao litakaposomwa tena.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri baada ya mabishano makali ya kisheria dhidi ya mawakili wa utetezi na mawakili upande wa jamhuri (serikali).

Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527