MAMIA WAFURIKA BANDA LA PSPF MAONESHO YA SABASABA YA 41 JIJINI DAR ES SALAAM



MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake (pichani juu), wamefurika kwenye banda la PSPF kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Undelezaji biashara nchini (Tan Trade) kwenye viwanja vya Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Wengi wa wananchi hao ni pamoja na wastaafu, wafanyakazi wa umma na binafsi ambao walifika kupata huduma mbalimbali lakini kubwa iliyovutia wengi kuuliza maswali ni jinsi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) unaomuwezsha mtu yeyote aliye kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi ili mradi awe na kazi inayomuinguizia kipato.

Akijibu maswali ya waliohitaji kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, Meneja wa Mpango huo, Bi. Mwanjaa Sembe alisema, kujiunga na mpango hyuo ni bure na mtu atakayejiunga atahitajika kuchangia shilingi kiwango chochote kila mwezi ambapo kiwango cha chini kabisa ni shilingi elfu kumi (10,000) tu.

Alisema mpango wa uchangiaji wa hiari licha ya kumuwezesha mwanachama kujiwekea akiba yake, lakini pia anafaidika na mafao mbalimbali ikiwemo fao la bima ya afya. Fao la elimu, fao la ujasiriamali, fao la uzeeni, fao la kujitoa na mikopo ya nyumba na viwanja, haya yote yatategemea na jinsi unavyojiwekea akiba (michango)
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kushoto), akipokea zawadi ambayo ni taarifa mbalimbali za Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutoka kwa Meneja wa Mpango wa uchangiaji wa Hiari, 9PSS), Bi. Mwanjaa Sembe, wakati alipotembelea banda la Mfuko huo Julai 1, 2017. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Mfuko huo, Bi Coletha Mnyamani.Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano ya Serikali wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja.
Afisa Uhusiano wa Mfuko huo, Bi Coletha Mnyamani, (kushoto), akimuhudumia mwananchi. 
Afisa wa Polisi aliyefika kujua michango yake akipatiwa huduma na Afisa uendeshaji wa PSPF, Bw.Miteko Chaula.
Afisa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Irine J. Musetti(kulia), akimfafanulia jambo mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la PSPF.
Bi Mwanjaa Sembe (kulia), akisalimiana na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Bi. Laura Kunenge, alipotembelea banda la PSPF 

Meneja wa Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe, (kulia), akimuhudumia mwananchi aliyefika kwenye banda la PSPF
Afisa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Irine J. Musetti akiwa kazini
Afisa uendeshaji wa PSPF, Bi. Asmahan H. Haji, (kulia), na Afisa uendeshaji msaidizi, Bw. Win-God Simon Mushi, wakitazama taarifa fulani kwenye kompyuta.
Afisa uendeshaji wa PSPF, Bi. Asmahan H. Haji, (kulia), akimuhudumia mwananchi aliyefika kwenye banda la Mfuko huo.
Afisa wa PSPF, Bw. Ali Sangura, (kushoto), akimpatia maelezo na ufafanuzi wa kina kuhusu huduma mbalimbali za Mfuko kwa wanachama wake, kwa mzee huyu mstaafu.
Afisa uendeshaji wa PSPF, Bw. Isack Kimaro, (kulia), akimsikiliza mwanachama huyu wa Mfuko aliyefika kujipatia huduma.

Na K-VIS BLOG/Khalfan Said

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post