MWENDESHA BODABODA AUAWA KWA KUCHINJWA KISHA KUPORWA PIKIPIKI

Mwanaume mmoja (30) mkazi wa Nyankumbu wilayani Nyamagana mkoani Geita anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la mauaji ya dereva bodaboda yaliyotokea majira ya 3:00 Usiku tarehe 06.05.2017.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Zarau Mpangule amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Andrea anayedaiwa kupora pikipiki na kumuua dereva wa pikipiki Bw. Alphonce Sekagi (32) mkazi wa wilayani Sengerema wakilishirikiana na wenzake wawili kisha kutoroka na pikipiki kusikojulikana.


Taarifa zinaeleza kuwa marehemu alikuwa dereva bodaboda wa mji wa Sengerema na siku ya tukio alipakia abiria watatu kwenye pikipiki yake wakitokea Sengerema mjini kwenda kijiji cha Tabaruka na kwamba wakati wakiwa njiani abiria hao walimkata dereva huyo na kitu chenye ncha kali shingoni kisha wakamchinja kwa kutumia panga shingoni na kupelekea kupoteza maisha papo hapo.


Kamanda Mpangule amesema wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanya msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi ndipo tarehe 01.06.2017 majira ya saa 8:30 mchana wakafanikiwa kumtamata mtuhumiwa mmoja akiwa na pikipiki waliyoipora katika mauaji hayo.


Kamanda Mpangule ameendelea kwa kusema upelelezi na msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine wawili ambapo wanadaiwa kushiriki katika mauji hayo pamoja na uporaji unaendelea huku mtuhumiwa aliyekamatwa anafanyiwa mahojiano na uchunguzi ukikamilika atapandishwa mahakamani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post