JE UPO TAYARI KUAMBUKIZWA UGONJWA KWA MAKSUDI ILI ULIPWE PESA KAMA KIFUTA JASHO?


Je ni pesa ngapi zinaweza kukushawishi kukubali kuambukizwa kikohozi ili kusaidia uvumbuzi wa kisayansi.

Watafiti katika chuo kikuu cha Southampton University wanawapatia watu pauni 3,526 ili kukubali changamoto hiyo.

Wanataka kutengeza chanjo bora ili kuwalinda watoto, na watu wazima ambao wapo hatarini kuambukizwa ugonjwa huo.

Ili kusaidia ni sharti uwe na umri wa kati ya miaka 18-45, uwe na afya bora, uwe tayari kutengwa kwa siku 17 na kuimba.

Kikohozi ni ugonjwa unaoweza kuambukizwa kwa haraka na huenezwa kupitia hewa ya kikohozi kutoka kwa mtu ambaye ameambukizwa .

Kundi hilo kutoka mjini Southampton linataka kuwaambukiza watu walio na afya nzuri kwa kuwawekea puani viini vinavyosababisha maambukizi hayo na kuwachunguza.

Baadhi ya watu waliojitolea watakuwa wagonjwa ,lakini wanasayansi wanataka wale ambao hawatakuwa na dalili zozote licha ya kuwekewa viini hivyo katika pua zao.

Kile wanachotafuta ni wale wanaobeba viini hivyo kwa siri na watu ambao wanakinga ya ugonjwa huo.

Wale wanaobeba ugonjwa huo kwa siri huwaambukiza watu wengine lakini huwa hawapatwi na ugonjwa huo.

Huonekana kuwa na kinga ya kutosha ya kukabiliana na ugonjwa huo licha ya kwamba hawajapewa chanjo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post