Utafiti: HISIA ZA MAPENZI ZINAMSAIDIA MUATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA AACHE KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha St George’s London wamegundua jinsi hisia za mapenzi zinavyoweza kumsaidia muathirika wa dawa za kulevya kupambana na hali ya arosto na kutaka kurudia matumizi ya dawa hizo iwapo aliacha kwa kipindi fulani.

Kwa mujibu wa utafiti huu binadamu huzalisha homoni inayoitwa Oxytocin ambayo humsaidia kuwa na hali ya furaha na raha ,homoni hii ambayo huzalishwa kwenye ubongo, itazalishwa kwa wingi iwapo mtu atampata mpenzi anayempenda.

Wanasayansi wanalinganisha raha na furaha anayoipata mtu akiwa na mtu ampendaye kuwa sawa na raha na furaha anayoipata mtu anayetumia dawa za kulevya kwani mtu anayetumia dawa hizo huzalisha homoni ya Oxytocin sawa na mtu aliyempata mpenzi mpya hivyo kumfanya asivute dawa za kulevya ili kuipata raha hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post