MANGU : POLISI,WANANCHI MPENI USHIRIKIANO IGP SIRRO

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewataka wananchi kumpa ushirikiano IGP mpya, Simon Sirro katika kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini hasa katika Mkoa wa Pwani.



Mangu aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es salaam baada ya Rais John Magufuli kumwapisha Sirro kuwa IGP mpya wa kuliongoza jeshi la polisi nchini.


Kuhusiana na hali inayoendelea mkoani Pwani, Mangu alisema "Sirro anafahamu anachotakiwa kufanya katika hilo, nimefanya naye kazi kwa karibu, ninachoomba ni askari na wananchi wote wampe ushirikiano"


Mangu ambaye anasubiri kupangiwa kazi nyingine alisema anamfahamu Sirro kama mchapakazi mzuri na ataweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na amani.


Sirro aliapishwa jana kuwa IGP, kabla ya uteuzi huo alikuwa kamanda wa polisi (RPC) katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Shinyanga. 


Baadaye alikwenda kitengo cha operesheni na mafunzo polisi makao makuu, kisha akahamishiwa kitengo hicho kanda maalumu ya Dar es Salaam kabla ya kuwa kamishna wa kanda hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527