MADHARA YANAYOWAPATA WATOTO WANAOLISHWA CHAKULA KWA KUTUMIA KIJIKO


Watoto ambao hulishwa chakula kwa kijiko wameelezwa kuwa hatarini zaidi kuwa na uzito mkubwa au unene kupita kiasi ukilinganisha na watoto ambao wanakula wenyewe kwa mikono yao, kwa mujibu wa utafiti mpya.

Amy Brown, Professor katika Chuo Kikuu cha Swansea amesema kuwa watoto wanaopewa nafasi ya kula wenyewe kwa mikono yao huwa na uwiano mkubwa wa afya bora hivyo wazazi wameshauriwa kutowalisha kwa kijiko watoto wenye umri wa zaidi ya miezi sita kwa sababu wanakuwa tayari wanaweza kula vyakula vigumu.

Akiongea na Sunday Times mwandishi huyo wa kitabu cha Why Starting Solids Matters, ambacho kitachapishwa wiki ijayo amesema lazima watoto waruhusiwe kula kidogo au zaidi pale wanapojifunza kula wenyewe akidai kuwa kutumia kijiko huwafanya watoto kula zaidi ya wanavyohitaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527