KUTANA NA PAKA MREFU ZAIDI DUNIANI

Paka huyu wa aina ya Maine Coon ana urefu wa sentimita 120

Omar alikuwa na ukubwa sawa na paka wengine wote waliokuwa wakiishi pamoja naye, kabla yake kuchukuliwa na mmiliki wake Stephy Hirst, mwaka wa 2013.

Lakini sasa paka huyu wa aina ya Maine Coon kutoka Melbourne, Australia ana urefu wa sentimita 120 (futi 3, inchi 11) na huenda akawa ndiye paka mrefu zaidi duniani aliyefugwa.

Baada ya sifa zake kuenea mitandaoni, Hirst anasema Guinness World Records waliwasiliana naye na kumuuliza kipimo cha paka wake.

Anayeshikilia rekodi kwa sasa ni paka aina ya Maine Coon kutoka Wakefield, West Yorkshire aliye na urefu wa sentimita 118 (futi 3, inchi 10.59).

Hirst alianza kuchapisha picha zake Omar kwenye mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita na moja kati ya picha hizo ilisambazwa zaidi ya mara elfu 270 katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Taarifa za Omar zimechapishwa kwenye magazeti nchini Australia na hata kwenye televisheni.

"Bado hajazoea umaarufu huu wote," Bi Hirst aliiambia BBC.

"Alikuwa ametatizika kidogo leo asubuhi."Omar pia ana talanta ya kufungua milango na kabati za nguo na vyombo.

Kwa kawaida Omar huamka saa kumi na moja asubuhi.

Yeye hula chakula chake na kisha kucheza nyumbani au uwanjani, kabla ya kupumzika. Chakula chake cha jioni huwa ni nyama ya kangaroo.

"Sisi hununua nyama ya kangaroo kwenye maduka makubwa makubwa, ni nyama sawa na ile inaliwa na binadamu," Bi Hirst alisema. "Hiyo tu ndio nyama anayoweza kula."

Mnyama huyo huwacha manyoya yake kila mahali anapopita ndani ya nyumba. Ana uzito wa kilogramu 14 na ni vigumu kumuinua kila mara.

"Yeye kuchukua nafasi kubwa kitandani na hivyo tunalazimika kumfungia nje ya chumba changu cha kulala usiku," Bi Hirst alisema.

Omar pia ana talanta ya kufungua milango na kabati za nguo na vyombo.

"Marafiki zetu wote hutaka kuja kumuona Omar," Bi Hirst alisema.

Baada ya Guinness World Records kudhibitisha ukubwa na urefu wake, inaweza kuchukua jumla ya wiki 12 kutoa majibu.

Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post