KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA ARUSHA SASA YAAMUA KUMSHUGHULIKIA RASMI DC MNYETI


Mwenyekiti wa Arusha Press Club (APC)Cloud Gwandu akizungumza katika siku ya maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani ,yaliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Rose Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mwandishi wa habari wa kituo cha Luninga cha ITV Khalifan Lihundi.

Katika kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani katika Mkoani wa Arusha,klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC) imekutana na wadau wa habari kujadili mambo mbalimbali yanayowahusu pamoja na changamoto mbalimbali wanazozipitia.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Arusha Club hiyo Cloud Gwandu amesema kuwa mkuu huo wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti alitoa amri ya kukamatwa kwa Mwandishi wa habari wa kituo cha luninga cha ITV Khalifan Liundi ,ambapo Mkuu wa mkoa na RPC wa mkoa husika wakiwa hawana taarifa .

"Tuliazimia kwa pamoja kuwa mkuu huyo wa wilaya atuombe radhi kwa kitendo hicho alichokifanya ,tulimpa miezi mitatu hadi sasa ni mwezi wa tano ,ninavyozungumza hapa hayafanya hivyo,badala yake akawa anawatumia wapambe tena wapambe nuksi kuja kwetu na kusema sisi tumfuate yeye ofisini kwake jambo ambalo halitawezekana " alisema mwenyekiti.


Hivyo Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha wamekubaliana kwa pamoja kutokuandika habari zozote zinazomuhusu mkuu huyo wa wilaya pamoja na shughuli zake zote anazozifanya kila siku.

Gwandu amesema kwa sababu miezi mitatu aliyopewa imepita ,mkuu huyo mwenye kiburi kuliko hajaomba radhi,klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha imeamua kuchukua hatua kwa kushirikiana na Wanasheria ili jambo hilo lifikishwe mahali panapostahili.

"Hivi karibuni aliitwa Bungeni na Kamati ya maadili ameomba radhi na amesamehewa kwetu sisi aliyetukosea hajaja kuomba radhi wala nini badala yake anataka sisi tumfuate ofisini kwake kumuomba yeye radhi,nasisitiza hivi tuendelee kususia kazi zake siyo za wananchi wa Arumeru bali za Alexander Mnyeti",alisisitiza Gwandu.

Ikumbukwe kuwa Mwandishi wa habari wa kituo cha Luninga cha ITV Khalfa Liundi alikamatwa mnamo tarehe 20 Disemba 2016 na kwa tuhuma za kuandika habari za uchochezi iliyokuwa ya malalamiko ya wananchi juu ya tatizo la Maji.
Na Vero Ignatus ,Arusha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post