KESI YA WEMA SEPETU KUTUMIA BANGI YAPIGWA KALENDA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeambiwa kwamba upelelezi wa kesi ya kukutwa na bangi inayomkabili Muigizaji maarufu, Wema Sepetu na wenzake umekamilika.


Hatua hiyo imefikiwa ambapo upande wa Jamhuri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema kwamba upelelezi umekamilika dhidi ya msanii huyo na wakili wa Serikali Helleni Mushi aliomba kesi hiyo kuarishwa na kupangwa tarehe ya kuanza kusikilizwa ili watuhumiwa waanze kusomewa maelezo ya awali.


Katika kesi ya msingi, Wema anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. 


Mbali na Wema washitakiwa wengine ni wafanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa (21) na Matrida Abas (16), ambapo wote wanashtakiwa kwa kosa moja la kukutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya.


Inadaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda kosa hilo Februari 4 mwaka huu, nyumbani kwao Kunduchi Ununio , Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.


Hakimu Simba alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa, Juni Mosi, mwaka kwa watuhumiwa kuanza kusomewa maelezo ya awali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post