KAULI ZA DR. KIGWANGALA BAADA YA RAIS MAGUFULI KUPOKEA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MCHANGA WENYE MADINI

May 24, 2017 Rais Magufuli amepokea ripoti ya Kamati ya Maalum iliyochunguza Mchanga wa Madini kwenye Makontena ambapo pamoja na mambo mengine yaliyogundulika JPM amemtaka Waziri mwenye dhamana kujitathmini.

Jambo hilo limegusa hisia za watu wengi mmoja akiwa ni Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangalla ambaye aliitumia account yake ya Twitter kuandika haya:
“Alichokifanya leo Rais Magufuli kwenye sekta ya madini ni jambo la kizalendo na kwa hakika litaleta mabadiliko, nilisema hivi tangu 2011.” – Kingwangala
President @MagufuliJP for what he is doing in the mining sector, is certainly a true patriot and a ! I said this in 2011! 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Sishangai kumsikia Rais wetu akisema 'Wasomi' tumeiangusha nchi. Kwa kila namna tunapaswa kujitazama sana! 
Ungeweza kusema 'wasomi' wetu hawakujua kama tunaibiwa (ignorance), walisoma nini sasa? Kwa vyovyote vile wawajibike tu! 
Ni ngumu sana kuamini kwamba 'wasomi' wetu hawakuwa wanajua kwamba tunaibiwa. Wabunge tulisema tukaonekana mbumbumbu! 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post