MUME AMUUA MKEWE KWA RISASI, NAYE AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI



Mkazi wa Mahina, jijini Mwanza, aliyefahamika kwa jina moja la Max, anadaiwa kumuua mke wake, Teddy Malulu kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo.
Baada ya kufanya mauaji hayo, Max naye anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi.

Mpaka sasa chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana. 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa mwanamke anayedaiwa kuuawa na mume wake ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Tanzania (Tafu) .

Kamanda Msangi amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post