RAIS MAGUFULI ATEUA WAJUMBE WA KAMATI YA PILI KUCHUNGUZA MADINI KWENYE MCHANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Aprili, 2017 ameteua wajumbe wa kamati maalum ya pili itakayofanya uchunguzi wa madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kamati hiyo inajumuisha wachumi na wanasheria na imetanguliwa na kamati ya kwanza iliyoundwa na wataalamu wa masuala ya jiolojia, kemikali na uchambuzi wa kisayansi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni;
  1.     Prof. Nehemiah Eliachim Osoro
  2.     Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara
  3.     Dkt. Oswald Joseph Mashindano
  4.     Bw. Gabriel Pascal Malata
  5.     Bw. Casmir Sumba Kyuki
  6.     Bi. Butamo Kasuka Philip
  7.     Bw. Usaje Benard Usubisye
  8.     Bw. Andrew Wilson Massawe
Wajumbe hao wataapishwa na Mhe. Rais Magufuli kesho tarehe 11 Aprili, 2017 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Aprili, 2017

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post