Utafiti : KULALA SANA KUNASABABISHA MTU KUNENEPA KUPITA KIASI


Kulala kwa masaa mengi au kwa muda mfupi vinaweza kuchangia mtu kunenepa kupita kiasi.

Utafiti umegundua kuwa usingizi usio mzuri unaweka mtu kwenye hatari ya kunenepa kupita kiasi kwa watu walio na maumbile ya kunenepa.

Hali hiyo ilishuhudiwa licha ya mtu kupata mankuli yanayostahili na kuwa na afya nzuri.

Watafiti waliangalia athari za kulala chini ya saa 7 kwa usiku na kulala masaa mengi zaidi, kama masaa tisa na hata kulala saa za mchana.

Waligundua kuwa watu wenye miili ya kunenepa , kulala kwa muda mfupi au masaa mengi, vyote vinachangia mtu kunenepa, ikilinganishwa na watu wanaolala muda unaotakikana wa kati ya masaa saba na nane.

Wanaolala masaa mengi na walio na miili ya kunenepa wanaweza kuwa na uzito wa kilo 4 zaidi, huku wale wanaolala muda mfupi wakipata uzito wa kilo 2 zaidi.

Takwimu hizo zilionyesha kuwa walio na jeni za kunenepa na wanaolala saa chache au saa nyingi, ambao hulala mchana na wakati wa mapumziko kazini, walionekana kuwa na athari kwa uzito wa miili yao.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post