Picha :MTANDAO WA JINSIA TANZANIA (TGNP) WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA


Mtandao wa Jinsia (Tanzania Gender Network Programme- TGNP) umetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga nakwa ajili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya kijinsia ili waweze kuandika habari zao kwa usahihi zaidi.


Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili (Machi 2 na Machi 3 mwaka 2017 katika ukumbi wa Vijana Center katika kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini Shinyanga pia yamewakutanisha waandishi hao wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa vilivyopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Mratibu wa mafunzo hayo ambaye pia ni mwezeshaji Bi Nyanjura Kalindo alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya kijinsia na kuwakutanisha na wanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ili kuongeza nguvu ya pamoja katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Vipaumbele vya TGNP ni vitano ambavyo ni afya,elimu,kilimo,uziduzi na maji hivyo kwa kuwapatia mafunzo waandishi wa habari tunaamini kabisa itaongeza chachu kuandika habari kwa usahihi zaidi kuhusu masuala ya kijinsia”,alieleza Kalindo.

Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bwana Rasel Madaha aliwaomba waandishi wa habari kufika katika maeneo ya pembezoni kwani vitendo vya ukatili wa kijinsia vipo na haviandikwi hali inayosababisha vitendo hivyo kuendelea kujitokeza na kuwafanya baadhi ya watu hususani watoto na wanawake kuendelea kunyanyasika.

Angalia picha wakati wa mafunzo hayo 
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Nyanjura Kalindo akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya kijinsia
Mwandishi wa habari gazeti la Nipashe Marco Maduhu akichangia mada wakati wa semina/mafunzo hayo.Kulia kwake ni wanaharakati wa kupinga ukatili wa kijinsia kutoka kata ya Mwadui-Luhumbo wilayani Kishapu wakiwa ukumbini
Mwezeshaji Nyanjura Kalindo kutoka mtandao wa jinsia Tanzania akitoa mada ukumbini
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Rasel Madaha akizungumza ukumbini
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Rasel Madaha akiwasisitiza waandishi wa habari kuandika habari zinazohusu watu wasio na sauti katika jamii
Mwandishi wa habari wa radio Free Africa Malaki Philipo (kulia) na Steve Kanyefu kutoka Radio Faraja fm stereo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na mwezeshaji Rasel Madaha
Mwezeshaji Rasel Madaha akiendelea kutoa mada
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na mwezeshaji wa mafunzo hayo Rasel Madaha
Mafunzo yanaendelea.Kulia ni mwanaharakati wa masuala ya jinsia kutoka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Kasigwa Adram,katikati ni mwandishi wa habari Sam Bahari akifuatiwa na Charles Jilala ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka wilayani Kishapu
Katikati ni mwandishi wa habari wa DW,Veronica Natalis akifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.Wa kwanza kushoto ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Elizabeth Joseph kutoka wilayani Kishapu
Mwandishi wa habari wa gazeti la Jamboleo Stephen Kidoyayi akichangia mada ukumbini.Kushoto ni mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja,bi Moshi Ndugulile
Katikati ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Rahel Madundo akiwa na washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Marco Maduhu akichangia mada wakati wa mafunzo hayo
Kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Stella Ibengwe akifuatiwa na Kareny Masasy wa gazeti la Habari leo na Wezay Ally kutoka radio Faraja 
Mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja Steve Kanyefu akichangia mada ukumbini
Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Rahel Lisesi kutoka wilayani Kishapu akielezea changamoto zinazowakabili wananchi wanaozunguka mgodi wa madini ya almasi wa Williamson uliopo Mwadui wilayani Kishapu
Mwandishi wa habari wa Azam TV,bwana Stephen Wang'anyi akichangia mada ukumbini.Kulia kwake ni mwandishi wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde
Mwandishi wa habari wa Malunde1 blog,Kadama Malunde akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru na Mzalendo,bwana Chibura Makorongo(aliyenyoosha mkono) akichangia hoja ukumbini
Kushoto ni mwezeshaji Nyanjura Kalindo akisisitiza jambo ukumbini
Mwandishi wa habari kutoka radio Faraja,Steve Kanyefu akichangia mada wakati wa mafunzo hayo
Kushoto ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia 
Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka wilaya ya Kishapu Charles Jilala akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata ya Mwadui-Luhumbo wilayani humo katika sekta ya afya,elimu,kilimo,uziduaji na maji
Mwandishi wa habari kutoka radio Faraja Simeo Makoba akiwa amenyoosha mkono kwa ajili ya kuchangia mada 
Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Rahel Madundo akielezea changamoto zinazowakabili wananchi wilayani Kishapu Picha ya pamoja baada ya mafunzo 
 Picha ya pamojaPicha ya pamoja ,wawezashaji wa mafunzo hayo,Rasel Madaha (kushoto) na Nyanjura Kalindo na Mwandishi wa habari wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC)

Picha na Frank Mshana,Stephen Wang'anyi na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post