Picha: MAZISHI YA MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN VALENCE ROBERT


Mazishi ya mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Channel Ten Valence Robert yamefanyika jana Machi 30,2017 katika kijiji cha Mgana wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.

Marehemu Valence Robert alianza kusumbuliwa na maradhi mwaka jana mwishoni na katika juhudi za kutafuta matibabu ambapo alipelekwa jijini Mwanza.

Alipatiwa matibabu na kurudia hali yake ya awali na kuendelea na majukumu yake ya kazi lakini mwanzoni mwa mwaka huu mwezi wa pili hali yake ya afya ilibadilika na kuzidiwa mwezi Machi hali ambayo ilimlazimu kurudi nyumbani kwa ajili ya matibabu.


Kwa Mujibu wa Mzazi wake wa kiume ,Mzee Robert Mulamula alisema hali yake ilibadilika ghafla siku ya Jumanne ya tarehe 28 na walipo kuwa katika jitihada za kutaka kumkimbiza hospitali hali ilibadiLika na kupelekea kukata kauli.


Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwilimu Herman Kapufi amewataka wazazi kuwa na moyo wa subira na kuachana na dhana ambazo zimekuwa zikiibuka pindi mtu anapofariki kuwa amelogwa na kwamba jambo hilo sio la kweli kwani marehemu alikuwa ni mgonjwa kama ambavyo wengine wamekuwa wakiugua.


Akimwakilisha Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo mkoani Geita Upendo Peneza katibu wake Shida Mpondi alisema mbunge huyo ameupokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani marehemu Valence Robert alikuwa ni mtu wa karibu ambaye walikuwa wakishirikiana katika kazi za ujenzi wa taifa.

Hata Hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Bugomola ,aliwaasa wanajamii ,ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu kuendelea kujikabidhi mikononi mwa Mungu kwani hayupo hajuae siku wala saa ya kuondoka Duniani.

Marehemu Valence Robart wakati wa uhai wake alikuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten na gazeti la Tanzania daima Mkoani Geita.

Alizaliwa Tarehe 9 mwezi wa 11 mwaka 1986 katika kijiji cha Mugana Wilayani Misenyi Mkoani Kagera akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya mzee Robert Mulamula na kufariki dunia tarehe 28 mwezi wa 3 mwaka 2017.
Baba wa Marehemu wa katikati akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye alifika kutoa pole na kushiriki mazishi.
Mkuu wa wilaya ya Geita akitoa pole kwa mama wa Marehemu Valence Robert.

Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi (katikati)akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita pamoja na mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita.
Mwili wa Marehemu Valence Robert ukitolewa nje.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ,akitoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu Valence Robert.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Lernad Kiganga Bugomola akitoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa mwanahabari Valence Robert.
Mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita,Saimon akiaga mwili.
Mwandishi wa ITV Mkoani Geita,Rose Mweko akitoaga mwili wa marehemu Valence Robert.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527