News Alert!! HATIMAYE MBUNGE GODBLESS LEMA APATA DHAMANA BAADA YA KUKAA MAHABUSU MIEZI 4

Hatimaye mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ameachiwa kwa dhamana kwa masharti ya wadhamini wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni moja.


Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo imesikiliza maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambaye alikuwa akiisaka kwa miezi minne.


Mbunge huyo ambaye alikamatwa tangu Novemba 2 mwaka jana akiwa bungeni Dodoma, aliwekwa mahabusu katika Gereza la Kisongo, Arusha.

Huu hapa ujumbe wa afisa habari wa Chadema Tumaini Makene aliopost Facebook
'Ushindi wa Godbless Lema leo ambao ni kielelezo cha ushindi wa Haki dhidi ya Udhalimu, ni mwanzo wa hatua nyingi kuanzisha mapambano dhidi ya mfumo kandamizi hasa matumizi mabaya ya notisi ya dhamana ambayo Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali imekuwa ikitumia kunyima haki ya dhamana watu wanaotuhumiwa makosa yanayostahili kudhaminiwa.

Ushindi wa Lema leo kutoka mahabusu kwa dhamana, umedhihilisha pasi na shaka kuwa wako Watanzania wanyonge, elfu kwa maelfu, haki zao zinaminywa na kunyimwa kwa makusudi kwa sababu ambazo watawala wanajua. Ni muhari sasa, Ofisi ya DPP isiendelee kunajisi taaluma ya sheria kama walivyosema Majaji wa Mahakama ya Rufaa Arusha. Haki si tu inapaswa kutendeka bali inapaswa kuonekana inatendeka'

Wafuasi wa Chadema wakiwa na tisheti zenye maneno ya upendo na uhuru kwa Lema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post