Breaking News! VIGOGO WA CCM WAFUKUZWA UANACHAMA CCM...WAMO WENYEVITI WA MIKOA..TAZAMA MAJINA YOTE HAPA


Maamuzi Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM leo Jumamosi  Machi 11,2017 Dodoma 

Kutoka Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma katika Mkutano Mkuu unaoendelea ni kwamba baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama huku wengine wakipewa onyo kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti/ukosefu wa maadili.

Miongoni wa waliofukuzwa uanachama ni pamoja na mwanachama mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba huku Adam Kimbisa akisamehewa na Emmanuel Nchimbi akipewa onyo kali.

Onyo kali alilopewa Nchimbi ina maana kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa miaka minne.

Kufuatia maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika.

 Hivyo, CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba nafasi ya Sophia, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.

Wengine waliovuliwa uanachama ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Madenge, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assa Simba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya, Mwenyekiti Mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa,Jesca Msabatavunga, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Ali Sumaye, Mjumbe wa NEC Arumeru, Mathias Manga.

Pia, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido Leiza amefukuzwa uanachama pamoja na Mwenyekiti wa CCM Arusha Mjini, Saileli Molleli, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Omary Hawadhi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Muleba, Mwenyekiti wa CCM Babati, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bunda, Mjumbe wa NEC Gureta.


Waliopewa onyo kali kwa makosa mbalimbali ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Abed Kiponza ambaye amepewa onyo kali na kuondolewa madarakani, Mjumbe wa NEC Mkoa wa Singida, Hassa Mzaha, Mwenyekiti wa UWT Gezabulu, Mjumbe wa NEC Kilwa, Ali Mchumo na Mjumbe wa NEC Tunduru, Chief Kalolo ambaye amevuliwa ujumbe huo na kupewa onyo kali.

SOMA HAPA VIZURI ZAIDI




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post