WAANDISHI WA HABARI WAWILI WAKAMATWA NA POLISI KILIMANJARO

 TAARIFA zilizotufikia hivi punde kutoka mkoani Kilimanjaro Kaskazini mwa Tanzania, zinaeleza kwamba waandishi wa Habari wawili wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani humo.


Waliokamatwa ni Rodrick Mushi wa Tanzania Daima na Gifti Mongi wa Gazeti la Majira na ZBC.

"Gift Mongi alikamatwa jana jioni na kuwekwa Mahabusu katika kituo cha Polisi Majengo huku Rodrick akikamatwa katika ofisi ya RPC akiwa na baadhi ya waandishi wenzake wakifuatilia kisa cha kukamatwa Gift" kimeeleza moja ya chanzo chetu

*****  Hii hapa taarifa kutoka Klabu waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro***** MECKI-ILIMANJARO PRESS CLUB.   
 Sakata la kushikiliwa na kuhojiwa waandishi wawili mkoani hapa Gift Mongi na Rodrick Mushi ni kweli ila bado   linashughulikiwa na idara ya upelelezi mkoa Kilimanjaro.

mpaka sasa hakuna aliyepo tayari kueleza kosa lao nini bali wanasisitiza makosa yao yanahusisha mikoa miwili Arusha na Kilimanjaro 

Na wanaendelea kuhojiwa baada ya kutuhumiwa wakihusisha pia watu wengine.

Ofisi ya RCO inasisitiza taarifa ya nini kimetokea na nini kimesababisha msemaji wake ni RPC lakini taarifa Za awali zinasema anaweza akaendelea kuhojiwa lakini si kwa sababu ya kazi yake ya uandishi ila kama mtu mwingine yeyote.

Suala la dhamana na taarifa nyingine Za ndani zinategemea kumalizika kwa upelelezi na italazimu kuhusisha mikoa ya Arusha na Kilimanjaro tunaendelea kufuatilia hatma ya suala hili hususan kauli ya RPC.


Tuvute subira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post