TAMKO LA CHAMA HA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA KUHUSU TUKIO MUME KUUA MKE WAKE DAR

TAMKO LA CHAMA HA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA ( TAMRA )
25.02.2017.

Tamko  la chama  cha  kutetea  haki za wanaume Tanzania kuhusiana na tukio la mauaji yaliyofanywa  na  Mohamed Mohamed mkazi wa  Boko Jijini Dar es salaam tukio ambalo limeteka hisia za wengi  kuwa mwanaume huyo ametenda kosa bila kuangalia pande zote ili kujua chanzo cha tatizo la wanandoa hao.


Chama cha kutetea haki za wanaume Tanzania TAMRA kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mauaji yaliyotokea huko Boko Dar  es salaam  kutokana na hatua zilizochukuliwa na mmoja wa wanaume aitwaye Mohamed Mohamed (46) mfanyabiashara mkazi wa boko  jijini dar es salaam kwa kumuua mkewe sophia(36) na kisha yeye mwenyewe kujiua na kuacha ujumbe kurasa 80 ujumbe ambao  kwa mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi ndiyo umebeba sababu mauaji hayo.

Kimsingi,jamii imekwenda mbali katika tukio hili kwa kuwachukulia wanaume kuwa ni wabaya,ni katili, sawa lakini chama hiki kinaomba jamii itambue uwepo wa migogoro mikubwa inayofukuta ndani ya ndoa zetu huku chanzo kikubwa kikiwa ni baadhi ya akina mama,nasema hivyo kutokana na ushahidi kwamba,tafiti zilizofanyika hapo nyuma zilionyesha kuwa katika mikoa minne ikiwemo lindi Mtwara, Dar es salaam na Zanzibar ilionyesha kuwa wanawake walikuwa wakiongoza kwa kupiga wanaume ikiwamo kuwanyima unyumba huku wanaume wakikosa pa kusemea kutokana na kutokuwepo kwa chombo hiki mpaka pale chama hiki kilipoanzishwa .
Matatizo mengine ukiachilia kupigwa wanaume wamekuwa wakipambana na vituko vingi ikiwemo ukatili wa kijinsia kwa kutengwa na familia wakiwemo watoto kuambatana na misimamo ya mama huku baba akibaki mkiwa na baadaye kupelekea vifo vingi kwa akina baba.

Tafiti zinaonyesha kuwa wanaoathirika zaidi ni wanaume hasa waliostaafu kazi serikalini taasisi na mashirika kwamba wanapokuwa wamekoma kupata fedha kwa ajiri ya kutunza familia hutengwa na baada ya muda huugua magonjwa makubwa ikiwemo kupooza,sukari,nk.

Yote haya yanatokana na mwanaume kushindwa kuthaminiwa utu wake na kudharauliwa na familia na hapo ndipo hujikuta katika lindi la mawazo na kupelekea kupoteza maisha.

Katibu mkuu wa chama cha kutetea haki za wanaume Antony Sollo amejaribu kufuatilia suala hili kuona jamii imelipokeaje tukio hili ambapo watu mbali mbali wameweza kuelezea hisia zao.


Akizungumza na katibu mkuu wa TAMRA Seif Hemed mkazi wa Uhuru jijini Mwanza ametoa maoni yake kuhusiana na tukio hilo na kusema kwamba tukio hili limesababishwa na mwanamke kutokana na majibu aliyokuwa akimjibu mwanandoa mwenzake hususani pale alipotamka kwamba watoto waliozaa si wake,matumizi mabaya ya fedha za mmewe jambo ambalo linaumiza moyo.


“Hata kama ningekuwa mimi nisingeweza kuvumilia kwa kuwa mke nimeshiriki kumtafuta kumlipia mahari,kumtunza kwa kumpatia mahitaji mbalimbali ikiwemo kulea ujauzito na kuwalea watoto nikijua ni mali yangu halafu leo mtu anaibuka na kusema kuwa watoto hawa si wangu inauma sana”, alisema Seif.

Kufuatia hali hii TAMRA haina ugomvi na wanawake ila inawataka wanandoa kuheshimu ndoa kwani ni agizo la mungu kwamba enendeni mkazaliane muijaze dunia ambapo baada ya agizo hilo muungu aliagiza mambo mawili ikiwemo wajibu wa kila mwanandoa.

Wwapo wanandoa watamheshimu mungu na kutekeleza wajibu wao kila mmoja ndoa hizo zitadumu na amani ndani ya ndoa hizo itakuwa ni ya milele.

Haya ni Maagizo ya mungu kwa wanandoa.
Kwa wanawake : WAEFESO 5 : 22 neno la Mungu linasema enyi wake watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu , kwa maana Mume ni kichwa cha Mkewe,kama kristo naye ni kichwa cha kanisa naye ni mwokozi wa mwili lakini kama vile kanisa limtiivyo kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

Kwa Wanaume: Waefeso 5: 25 Enyi waume wapendeni wake zenu kama kristo naye alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajiri yake,ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno apate kujiletea kanisa tukufu lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayobali liwe takatifu lisilo na mawaa vivyo hivyo imewapasa waume zao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe,hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote bali huulisha na kuutunza kama kristo naye alivyolitendea kanisa.

Hivyo nachukua nafasi hii kuiomba jamii mambo yafuatayo:
1.      Kuheshimu neno la Mungu ili kuweza kudumisha ndoa zetu.
2.      Kuwa wavumilivu katika shida na raha kama viapo tulivyoapa mbele za Mungu
3.      Tuweze kujifunza masomo ya ndoa ili kuingia katika ndoa tukiwa na ujuzi juu ya wajibu wetu baada ya kuingia katika Tasnia hii muhimu ya ndoa.

4.      Tumtegemee Mungu katika mambo yote na tukio hili liwe fundisho kwetu tujipeleleze ni wapi tuna Mgogoro usioisha katika ndoa zetu ili kuepuka Mauaji ya aina hii.

IMEANDALIWA NA:
Antony Johnson Sollo
KATIBU MKUU TAMRA TANZANIA
1.      0767 203 556  BERENS CHINA                        Mwenyekiti  TAMRA
2.      0762  117 117  ANTONY JOHNSON SOLLO  Katibu Mkuu TAMRA


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post