MWANAMKE AKATWA MASIKIO NA MUMEWE

Mwanamke mmoja wa miaka 23 kutoka nchini Afghanistan ameielezea BBC kwamba mumewe alimfunga kamba na kumkata masikio yote mawili katika mzozo wa kinyumbani katika mkoa wa kaskazini wa Balkh.

Mwanamke huyo Zarina kwa sasa yuko katika hali nzuri hospitalini.

''Sijatenda dhambi lolote'' ,alisema.''sijui kwa nini mume wangu alinifanyia hivi''.

Mume huyo kwa sasa ameenda mafichoni katika Ulaya ya kashinda kufuatia shambulio hilo kulingana na maafisa wa polisi.

Zarina ameambia chombo cha habari cha Pajhwok kwamba shambulio hilo ambalo anasema halikusababishwa na hatua yoyote lilifanyika baada ya mumewe kuamka.

Mwanamke huyo aliolewa akiwa na umri wa miaka 13 na ameiambia BBC kwamba uhusiano wake na mumewe haukuwa mzuri.

Zarina alilalamika kwamba mumewe alijaribu kumzuia kutowatembelea wazazi wake, amesema hataki kuwa naye tena.

"Ananishuku sana na kila mara unituhumu kwa kuzungumza na wanaume wengine wakati ninapoenda kutembelea wazazi wangu'' ,alisema.

Ametaka akamatwe na kushtakiwa.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post