Makubwa Haya!! MZEE WA MIAKA 78 AANZA KUSOMA DARASA LA KWANZA TARIME..TAZAMA PICHAMzee anza darasa la kwanza
Mzee Nyamhanga Suguta (78) mkazi wa kijiji cha Getenga kata ya Mbogi wilaya ya Tarime mkoani Mara akiwa ndani ya darasa la kwanza katika shule ya msingi Makerero baada ya kuamua kuanza kusoma darasa la kwanza
mzee aanza kusoma darasa la kwanza
Mzee akiwa paredi na wanafunzi wenzake
Mzee Nyamhanga Suguta (78) mkazi wa kijiji cha Getenga kata ya Mbogi wilaya ya Tarime mkoani Mara akiwa ndani ya darasa la kwanza
Muda wa kwenda nyumbani mzee akiwa paredi
******
Mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la Nyamhanga Suguta Gesaba (78) mkazi wa kitongoji cha Kibeyo Kijiji cha Getenga kata ya Mbogi Wilayani Tarime Mkoani Mara ameamua kujiunga na masomo ya shule ya msingi na kuanza darasa la kwanza katika shule ya msingi Makerero.


Mzee huyo anasema lengo kuanza kusoma ni kujua kusoma ,kuandika na kuhesabu ili kuendeleza biashara zake ndogo ndogo za kuuza ndizi.


Mzee Huyo amesema kuwa hakubahatika kwenda shule kipindi cha ujana wake hivyo alianza mwaka jana kwenda shule na akabahatika kufaulu na hivyo ameamua kujiunga darasa la kwanza ili kutimiza ndoto yake kwani elimu haina mwisho.

Walimu wa mwanafunzi huyo wanasema maendeleo yake shuleni ni mazuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post