Picha: RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA SHINYANGA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 53 MAPINDUZI YA ZANZIBAR



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Alhamis Januari 12,2017 amewahutubia wananchi wa mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Magufuli amesema kuanzia sasa sikukuu zote za kitaifa zitakuwa zinaadhimishwa katika maeneo mbalimbali nchini badala ya kulundikana sehemu moja kama ilivyofanyika leo kwani maadhimisho mengine ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yameendelea Zanzibar.

Rais Magufuli aliutaka uongozi wa mkoa wa Shinyanga,wizara ya fedha,wizara ya viwanda na Biashara kutafuta mwekezaji mwingine wa kuendeleza kiwanda cha nyama kilichojengwa mwaka 1970 na mpaka sasa hakifanyi kazi kutoka na mwekezaji Tripple S kushindwa kukiendeleza.

Kuhusu kero ya bei kubwa ya maji katika manispaa ya Shinyanga,rais Magufuli alisema atamtuma waziri wa Maji na Umwagiliaji kuja kufuatilia bei ya maji inayotozwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga KASHWASA na kulinganisha na sehemu zingine nchini na ikibainika kuwa ni kubwa bei itashushwa.

Aidha alisema serikali itajenga kiwanja cha ndege cha mkoa wa Shinyanga kwa kiwango cha lami ili ndege zilizonunuliwa na serikali ziweze kutua mkoani Shinyanga. 

Rais Magufuli pia aliwataka wananchi kulima mazao yanayostahili ukame huku akiwashukuru walimu katika shule za msingi na sekondari kusimamia vyema pesa za ruzuku zinazotumwa na serikali kwa ajili ya kufanikisha elimu bure kwa wanafunzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Shinyanga baada ya kuwasili katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Alhamis Januari 12,2017-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuwasili katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga leo Alhamis Januari 12,2017
Rais Magufuli akiangalia kikundi cha Ngoma kutoka Shinyanga Vijijini
Rais Magufuli akiwasalimia wananchi wa mkoa wa Shinyanga,aliyevaa suti nyeusi na ushungi mweupe (kulia kwake) ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Rais Magufuli akiwasalimia wakazi wa Shinyanga waliofika katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga,aliyevaa suti nyeusi na ushungi mweupe (kulia kwake) ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wakazi wa Shinyanga wakiwa uwanjani
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitambulisha wageni mbalimbali waliofika katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akizungumza uwanjani ambapo alifikisha kilio cha wakazi wa Shinyanga cha muda mrefu kuhusu Kiwanda cha Nyama cha Old Shinyanga ambacho hakifanyi kazi tangu kianzishwe mwaka 1970
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal (CCM) akielezea kero zinazowakabili wakazi wa Shinyanga na kumuomba rais Magufuli asaidie katika kutatua kero hizo ambazo ni pamoja na barabara na hospitali.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele (CCM) akielezea jinsi kero ya bei kubwa ya maji katika manispaa ya Shinyanga ambayo imekuwa ikitozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (KASHWASA).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akielezea kuhusu umuhimu wa Mapinduzi ya Zanzibar yaliyosababisha kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Waziri wa TAMISEMI Zanzibar Haji Omari akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema maadhimisho ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar yamefanyika kwa mara ya kwanza Tanzania bara katika mkoa wa Shinyanga mwaka huu 2017 na kuwataka watanzania kuendelea kudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Rais Magufuli akiwahutubia wakazi wa Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Stephen Masele akieleza mbele ya rais Magufuli kuhusu kero ya bei kubwa ya maji kwa wakazi wa Shinyanga 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga Injinia Sylivester Mahole akieleza kuhusu bei za maji mbele ya rais Magufuli ingawa hata hivyo aliishia kuzomewa na wananchi hali iliyosababisha rais Magufuli kumtoa jukwaani
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akionesha kitita cha fedha taslimu shilingi Milioni moja zilizotolewa na rais Magufuli kwa ajili ya wasanii mbalimbali waliotoa burudani uwanjani
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Muliro Jumanne Muliro (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali uwanjani

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post